Psalms 105:1-15

Uaminifu Wa Mungu Kwa Israeli

(1 Nyakati 16:8-22)

1 aMshukuruni Bwana, liitieni jina lake,
wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.
2 bMwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa,
waambieni matendo yake yote ya ajabu.
3 cLishangilieni jina lake takatifu,
mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi.
4 dMtafuteni Bwana na nguvu zake,
utafuteni uso wake siku zote.

5 eKumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya,
miujiza yake na hukumu alizozitamka,
6 fenyi wazao wa Abrahamu mtumishi wake,
enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
7 gYeye ndiye Bwana Mungu wetu,
hukumu zake zimo duniani pote.

8 hHulikumbuka agano lake milele,
neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,
9 iagano alilolifanya na Abrahamu,
kiapo alichomwapia Isaki.
10 jAlilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri,
kwa Israeli liwe agano la milele:
11 k“Nitakupa wewe nchi ya Kanaani
kuwa sehemu utakayoirithi.”

12 lWalipokuwa wachache kwa idadi,
wachache sana na wageni ndani yake,
13 mwalitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine,
kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
14 nHakuruhusu mtu yeyote awaonee;
kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema:
15 o“Msiwaguse niliowatia mafuta;
msiwadhuru manabii wangu.”
Copyright information for SwhNEN